Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amekanusha taarifa zinazoeleza kuwepo na tofauti katika vyumba vya kubadilishia ngo vya klabu hiyo kama ambavyo vyanzo mbalimbali vinaeleza.
Ten Hag ameweka wazi kua hakuna chochote kinachoendelea tofauti ndani ya vyumba vya kubadilishia ngo vya klabu hiyo, Huku akisema kuna umoja mkubwa kuanzia kwa jopo la makocha,madaktari na wachezaji wa timu hiyo.Taarifa mbambali ndani ya Manchester United zilieleza kua ndani ya vyumba vya kubadilishia vya klabu hiyo kuliibuka hali ya utofauti ambapo baadhi ya wachezaji waliingia kwenye utofauti kitu ambacho kocha huyo amekanusha.
Klabu hiyo pia inaelezwa wachezaji hawakubaliani na kocha kumuondoa kwenye timu winga wa klabu hiyo Jadon Sancho, Lakini tetesi zote hizi kocha huyo amekanusha leo kwa kusema timu hiyo iko pamoja na wanawaza kushinda tu mchezo wao unaofuata.Kocha Erik Ten Hag amewahakikishia wanahabari timu hiyo ipo kwenye utulivu mkubwa na kusema anawajua wachezaji wake vizuri, Hivo wanahabari waachane na tetesi au zinazoitwa habari za kuvuja kwakua akili yao kwasasa ipo inawaza kushinda mchezo unaofuata.