Ten Hag Ammwagia Misifa Onana

Baada ya Golikipa Andre Onana kutangazwa rasmi jana kama golikipa mpya wa klabu ya Manchester United kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag amemmwagia sifa kedekede kipa huyo.

Kocha Ten Hag wakati akiongea na Manchester Tv amesema kua kazi kubwa ya golikipa ni kufanya goli kua salama, Lakini vilevile mpira umebadilika unahitaji kipa mwenye uwezo wa kucheza kuanzia nyuma na Onana ana ubora huo.ten hagAndre Onana amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Manchester United akitokea Inter Milan ya nchini Italia ambapo alionesha ubora mkubwa ambapo klabu ya Man United ilivutiwa kumrudisha klabuni hapo.

Kocha Ten Hag ameonesha furaha yake juu ya Onana kujiunga na klabu hiyo kwani anaujua ubora wake kwakua ameshamfundisha golikipa huyo wakati wote klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi ambapo walifanikiwa kwa pamoja.ten hagKama ambavyo ameeleza kocha Ten Hag mpira wa kisasa unahitaji sana golikipa ambaye ana uwezo wa kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma kutokana na uwezo wake wa kupiga pasi, Huku ikiwa ndio sababu kubwa ya David De Gea kuondoka klabuni hapo kutokana na kukosa ubora huo.

Acha ujumbe