Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag ameweka wazi kua anahitaji kikosi kipana na chenye ubora ili kuweza kupata matokeo bora mfululizo kipindi hichi ambacho klabu hiyo inapata matokeo yasiyoridhisha.
Manchester United jana ilipokea kipigo cha mabao matatu kwa bila kutoka kwa klabu ya Bournamouth katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford jambo ambalo limemuibua kocha Erik Ten Hag na kuzungumza.Kocha huyo anasema ili kuweza kupata matokeo bora mfululizo ni kuhakikisha basi klabu hiyo inapaswa kua na kikosi kipana chenye ubora haswa kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Kocha huyo wa zamani wa Ajax amesema katika ligi kuu ya Uingereza kama hautacheza kwenye kiwango cha juu basi lazima utaadhibiwa tu na kuishia kupoteza mchezo, Hivo ili kutatua hilo unapaswa kupata kikosi chenye ubora mkubwa ambacho kinaweza kushindana.Kocha Erik Ten Hag ameeleza wazi hajafurahishwa na matokeo ya mchezo wa jana dhidi ya Bournamouth cha mabao matatu kwa bila, Huku akiongeza alitarajia kitu cha tofauti zaidi ya ambacho amekivuna katika mchezo huo.