Ten Hag Awavutia Mabosi Wote Wanaoiwania Klabu Hiyo

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag inaelezwa amewavutia mabosi wote wanaoitaka klabu hiyo kutokana na mwenendo wake ndani ya klabu hiyo tangu aichukue tiimu hiyo mwaka jana mwezi Juni.

Mabosi wawili wanaoiwania klabu hiyo Sheikh Jassim kutoka Qatar na Sir Jim Ratcliff raia wa Uingereza wote wanaelezwa kuvutiwa na Ten Hag, Hivo mmoja wao akichukua timu ataendelea kuweka imani yake kwa kocha huyo ambaye anaonekana kufanya vizuri klabuni hapo.Ten HagKocha huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekua akionesha mabadiliko makubwa ndani ya timu hiyo tangu kuchukua timu hiyo mwezi Juni mwaka jana, Akifanikiwa kuitengeneza timu hiyo na kuifanya kua moja ya timu bora kwasasa nchini Ulaya na kuingia ndani ya timu nne za juu mpaka sasa ikikamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Kocha Ten Hag amefanikiwa kuifanya Man United kushinda taji la kwanza mwaka huu baada ya kukaa kwa takribani miaka sita bila kubeba taji lolote, Lakini baada ya ujio wa kocha huyo wamefanikiwa akushinda taji la Carabao mwezi Febuari mwaka huu.Ten HagKlabu ya Manchester United chini ya Ten Hag mpaka sasa ni klabu namba moja kwa kushinda michezo mingi katika michuano yote ndani ya ligi kuu tano bora ulaya, Hivo hii inaendelea kuonesha sababu kwanini kocha huyo ameweza kupata imani ya mabosi wote wawili wanaowania klabu hiyo.

Acha ujumbe