Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema kua kiungo wa klabu hiyo Carlos Casemiro ameongeza ari ya ushindani kwenye klabu hiyo tangu amejiunga hapo.
Ten Hag anaamini kua Casemiro amefanikiwa kuongeza hali ya ushindani vilevile anaona nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya klabu hiyo kwasasa na hata kombe ambalo wamelibeba juzi kiungo ana mchango mkubwa.Kiungo Casemiro amekua kwenye kiwango bora ndani ya klabu ya Manchester United tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Real Madrid amekua mhimili mkubwa ndani ya timu hiyo, Huku akifanikiwa kumaliza tatizo la kiungo wa ulinzi lililoisumbua klabu hiyo kwa muda mrefu.
Kocha Ten Hag amesema kua klabu ya Manchester United inajivunia kua na Casemiro bdabi ya klabu hiyo kutokana na ubora ambao ameuleta ndani ya klabu hiyo, Lakini pia ameongeza hamasa kwa wachezaji wengine kutokana na mchezaji huyo kua mshindani.Carlos Casemiro amefanikiwa kuingia kwenye kikosi bora cha mwaka cha shirikisho la soka duniani FIFA mwaka 2022 na hiyo inatokana na kua na kiwango bora kwa mwaka 2022 akiwa na vilabu viwili klabu ya Real Madrid pamoja na Manchester United.