Ten Hag Haeleweki na Man United Yake

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag bado haeleweki na timu yake kwani bado anaonekana kusuasua kwenye kupata matokeo ndani ya timu hiyo na hii imekuja baada ya kulazimishwa sare jana wakiwa nyumbani.

Manchester United msimu huu imeonekana kuanza vibaya mpaka sasa kwani kwenye michuano yote mpaka sasa wamecheza michezo saba, Huku wakipata matokeo ya ushindi mechi tatu wakisuluhu michezo miwili na kufungwa miwili ikiwa sio mwanzi mzuri kwa klabu kariba ya Man United.ten hagJana klabu hiyo ilianza kampeni yake kwenye michuano ya Uefa Europa League wakiwa katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Fc Twente kutoka nchini Uholanzi na kuishia kupata sare ya bao moja kwa moja, Hii ikiwa ni muendelezo wa matokeo yasiyoridhidha ndani ya klabu hiyo kwa msimu wa 2024/25.

Klabu ya Manchester United kwenye michezo yake tisa ya mwisho ya ulaya wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee, Huku wakifungwa michezo mitano na kusuluhu michezo mitatu jambo ambalo linaendelea kuonesha muenendo mbaya wa klabu hiyo ambao umekua ukiwachanganya mashabiki wa klabu hiyo.

Kocha Erik Ten Hag ni wazi mpaka sasa ameonekana kushindwa kutengeneza mfumo sahihi ambao utaweza kuwafaa wachezaji wa klabu hiyo kuweza kucheza viwango vya juu, Kwani wachezaji wanaonekana wazuri ndani ya timu hiyo na usajili umefanyika tofauti misimu mitatu nyuma lakini kocha huyo ameshindwa kupata kitu bora kutoka kwa wachezaji wake mpaka sasa.

Acha ujumbe