Kocha wa klabu ya Manchester Erik Ten Hag ameweka wazi kua hali ni shwari ndani ya timu hiyo tofauti na inavyoelezwa kua kuna matatizo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Ten Hag amesema wachezaji wako sawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na akiamini wachezaji hao wataamka na kuanza kufanya vizuri kama ambavyo walifanya mwaka jana kwakua wako chanya.Kocha huyo ametupilia mbali taarifa zinazoeleza kua ndani ya timu hiyo kuna fukuto na baadhi ya wachezaji wameanza kutokua na imani na mbinu zake, Lakini kutokana na kauli yake aliyoitoa leo inaonesha wazi hakuna tatizo kwenye timu.
Manchester United imekua kwenye kiwango kibaya zaidi msimu huu na kusababisha kocha huyo kuanza kufikiriwa amefeli kwenye timu hiyo, Lakini uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi bado una imani na kocha huyo raia wa kimataifa wa Uholanzi.Kocha Erik Ten Hag alienda mbali na kusema kutokana na wachezaji kua sawasawa katika vyumba vya kubadilishia nguo, Lakini yeye kama mwalimu ndio anapaswa kuwajibika kuhakikisha wachezaji wake wanacheza vizuri.