Ten Hag: Hatuwezi Kugombea Ubingwa Msimu Ujao

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag ameweka wazi kua klabu hiyo haina uwezo wa kugombania ubingwa msimu ujao zaidi watagombea nafasi nne za juu.

Kocha Ten Hag ameyazungumza hayo mbele ya waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa ligi kuu ya Uingereza utakaopigwa leo dhidi ya klabu ya Burnley wakiwa katika dimba la Old Trafford.ten hagKocha huyo amezungumza hivo kutokana na kuangalia mwenendo wa klabu hiyo hivi karibuni, Lakini pia akieleza nafasi ambayo wanaweza kuipambania ni nafasi nne za juu ambazo msimu huu wanaonekana kama tayari wamezikosa.

Manchester United imekua haina msimu mzuri sana wakipoteza michezo mara kwa mara, Lakini pia majeraha yamekua moja ya matatizo yao msimu huu kwani wachezaji wao muhimu wamekua wakipata majeraha mara kwa mara.ten hagKocha Ten Hag pia alisema klabu hiyo kama itafanya usajili mzuri katika dirisha kubwa wanaweza kukaribia nafasi ya kwanza na ya pili, Ieleweke kocha huyo amesema kukaribia na sio kukaa na ndio maana ameweka wazi kabisa mapema kua watagombania nafasi nne za juu.

Acha ujumbe