Kocha mkuu wa Manchester United Erik Ten Hag ametwaa tuzo ya kocha bora ya mwezi Septemba katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kushinda mechi zake nne mfululizo ikiwemo kuvichapa vilabu vikubwa ndani ya EPL ambapo ni Liverpool na Arsenal.
Ten Hag alianza vibaya msimu huu ambapo alipoteza mechi za kwanza za ufunguzi wa kampeni yake ikiwemo mechi ya Brighton na Brentford huku wakiwa wamefanya usajili wa wachezaji mbalimbali ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi chao.
United msimu uliopita ilishindwa kufuzu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, ambapo ni michuano pendwa Duniani na akaangukia kucheza Uropa ambapo mechi yake ya kwanza alipoteza dhidi ya Real Sociedad na kupata ushindi kwenye mechi ya pili dhidi ya Sherrif.
Ten Hag wikiendi hii atacheza dhidi ya Manchester City ambapo itakuwa ni Dabi ya jiji la Manchester huku ikionekana kuwa vijana wa Pep Guardiola ndio wanaweza kuondoka na ushindi huku Haaland akitarajiwa kufanya vitu vikuwa kwenye mechi hiyo siku ya Jumapili.