Kocha wa Manchester United Eric ten Hag ameingia kwenye orodha ya makocha wanaowania tuzo ya kocha bora wa mwezi wa tisa katika ligi kuu ya Uingereza.

Mdachihuyo aliejiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akichukua mikoba ya kocha wa muda Ralf Rangnick amejumuishwa kwenye orodha ya makocha wanaowania tuzo hiyo baada ya kufanya vizuri na timu yake ndani ya mwezi wa tisa baada ya kuiongoza timu hiyo kushinda michezo yote ndani ya mwezi wa tisa.

Ten hagKocha huyo anaungana na makocha wengine wawili kutoka klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte na kocha wa klabu ya Afc Bournamouth aliechukua mikoba ya Scott parker Gary Oneil.

Eric ten Hag amefanikiwa kushinda michezo miwili aliyocheza ndani ya mwezi wa tisa kwenye ligi kuu nchini Uingereza akikusanya alama sita sawa na Antonio Conte huku Gary wa Bournamouth akishinda mchezo mmoja na kusuluhu mmoja.

Kocha huyo ameanza kufanya vizuri ndani timu hiyo baada ya kuanza msimu vibaya kwa kupoteza michezo yote miwili ya awali kwenye ligi hiyo na kushinda michezo yote minne iliyofuatia katika ikiwa ni pamoja na kuwafunga vigogo kama Liverpool na Arsenal.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa