Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema kua anapenda mpira ambao unavutia watu na sio mpira ambao unakera watu ameyazungumza hayo baada ya kushinda mchezo wa jana dhidi ya klabu ya Barcelona.

Kocha Ten Hag anasema falsafa yake ya mpira inafahamika na anapenda sana mpira wa kubadilika huku akisema hapendi mpira ambao utakua hauvutii watu kuwatizama, Akisema mpira ambao amekua akiupa kipaumbele kwake ni mpira unaowavutia watu kuutizama.Erik Ten HagKocha huyo anafahamika kutokana na uwezo wake wa kutengeneza timu ambayo inacheza mpira wa kuvutia na wenye kasi akifanikiwa kufanya hivo akiwa katika klabu ya Ajax, Huku kawasasa akifanikiwa kuitengeneza klabu ya Manchester United na kuonekana timu inayocheza mpira wa kasi.

Ten Hag kwa kipindi cha miezi saba tayari amefanikiwa kuifanya klabu ya Manchester United kua moja ya klabu tishio ndani ya ligi kuu ya Uingereza kwani mpaka sasa klabu hiyo imefanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye ligi kuu ya Uingereza ikiwa nyuma kwa alama tano nyuma ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Arsenal.Erik Ten HagKocha huyo raia wa kimataifa wa Uholanzi mpaka sasa amekua na wastani mkubwa wa ushindi kuliko kocha yeyote ambaye amewahi kupita katika klabu ya Manchester United, Hali hii inaonesha kua Ten Hag ana kila dalili ya kuirudisha klabu ya Manchester United kwenye ubora wake.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa