Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema mchezaji wake Jadon Sancho kwasasa kuna hatua amepiga baada ya kukosekana uwanjani kwa muda mrefu.
Mchezaji Jadon Sancho amekosekana ndani ya klabu ya Manchester United tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka jana, Siku mbili zilizopita ameonekana kurejea kwenye mazoezi ya klabu hiyo na kocha Erik Ten Hag akionekana kuzungumzia maeneleo yake.
Kocha Ten Hag amesema kua kuna hatua amepiga mchezaji Jadon Sancho ambaye amekua nje ya timu hiyo kwa muda wa karibu miezi miwili sasa akifanya mazoezi binafsi, Hiyo ilikua programu maalumu ambayo alikua akifanya mchezaji huyo ili kuweza kumjenga na jurudisha ubora wake.
Mchezaji Jadon Sancho ambaye amejiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2021 akitokea Borussia Dortmund amekua akisuasua ndani ya klabu hiyo na kushindwa kuonesha ubora ambao unahitajika, Ndipo kocha wake kumtaka kufanya mazoezi maalumu ili kurejesha makali yake.
Kocha Erik Ten Hag pia aliweka wazi mchezaji huyo alifanya mazoezi na timu ya kwanza siku ya jumanne kwa mara ya kwanza tangu mwezi Novemba, Lakini mchezaji huyo asingeweza kuwepo kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace kutokana na kua alifanya mazoezi siku moja na timu hiyo lakini kocha ameweka wazi kuna maendeleo anayaona kwa mchezaji huyo.

