Ten Hag: Tunakwenda Kushinda Dhidi ya Liverpool

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema anaamini kua wanaenda kushinda mchezo wao dhidi ya klabu ya Liverpool unaotarajiwa kupigwa katika dimba la Anfield leo.

Kocha Ten Hag anasema ameiandaa timu kwenda kucheza mchezo huo kwakua anaamini wana uwezo wa kwenda kushinda mchezo huo, Kauli ya kocha huyo imestaajabisha watu wengi.ten hagWakati kocha huyo akiamini wanakwenda kushinda mchezo dhidi ya Liverpool wengi wameshtuka kutokana na kauli ya kocha huyo, Kwani Man United wamekua hawana matokeo ya kuridhisha siku za karibuni wakati huo Liverpool ni vinara wa ligi kuu ya Uingereza.

Mchezo kati ya Manchester United na Liverpool umekua mgumu kila mara timu hizo zinapokutana, Lakini rekodi zinaibeba Liverpool kuelekea mchezo huo haswa katika uwanja wao wa nyumbani wa Anfield ambapo Man United hawajashinda tangu 2015.ten hagKocha Ten Hag amesema anaamini wanakwenda kshinda kutoka na kanuni na taratibu za mchezo lakini pia mpango wao waliouandaa kuelekea mchezo huo, Kikubwa zaidi ameeleza ana imani kubwa na ubora wa wachezaji wake.

Acha ujumbe