Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema kua watarejea kwenye ubora wao licha ya mfululizo wa matokeo mabaya ambayo wameyapata hivi karibuni.
Ten Hag anaamini ni suala la muda tu wao kuanza kuonesha makali yao kwakua klabu hiyo ina presha kubwa sana, Lakini akiamini watarejea kwenye ubora wao na wanalifanyia hilo kazi.Klabu ya Manchester United mpaka sasa imeshapoteza nusu ya michezo waliyocheza kwenye ligi kuu ya Uingereza, Ambapo wamecheza michezo 10 huku wakiwa wameshapoteza michezo mitano jambo ambalo sio zuri kwa klabu hiyo.
Kocha huyo anaeleza kua wanapambana kuhakikisha wanarudia kwenye ubora wao ambao waliuonesha msimu uliomalizika, Kwani msimu uliomalizika Man United walikua kwenye ubora na wengi wakiamini msimu huu ndio wangekua vizuri zaidi lakini mambo yamekua tofauti.Manchester United imekua na msimu mbaya sana na mfululizo wa matokeo mabaya jambo ambalo limefanya mashabiki wa klabu hiyo kuanza kufikiria kocha Ten Hag amefeli klabuni hapo, Lakini kocha huyo amethibitisha kua watarejea kwenye ubora wao hivi karibuni.