Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema kwa kipindi kirefu Manchester United imekua ikifanya usajili wa wachezaji wa kawaida.

Kocha huyo amezungumza hayo baada ya kupata ushindi katika mchezo wa kombe la FA siku ya jana dhidi ya klabu ya Everton kwa mabao matatu kwa moja. Kocha huyo anaamini klabu hiyo ilikua ikiingia sokoni na kufanya usajili wa wachezaji wengi ambao ni wa kawaida.Ten HagKocha Erik Ten Hag anasema jezi ya klabu ya Manchester United ni nzito na unahitaji kupata mchezaji mwenye uwezo wa kucheza kwenye presha kubwa, Huku imani yake yeye ni kuamini kua timu hiyo inahitaji wachezaji wa daraja la juu ambao wataendana na ukubwa wa klabu hiyo.

Kocha huyo anaonekana ni kocha ambaye yupo makini na muwazi kwenye kile ambacho anakiamini na ndio sababu mara nyingi amekua akiweka wazi mambo ambayo amekua akiona yako tofauti, Na hata suala nidhamu kwa wachezaji ndani ya klabu hiyo amekua akilisimamia kwa umakini mkubwa.Ten HagErik Ten Hag anaonekana kufanya vizuri ndani ya klabu hiyo mpaka sasa huku mashabiki wengi wakiamini kocha huyo akipewa ushirikiano na uongozi wa klabu hiyo basi anaweza kurudisha zama bora za klabu hiyo. Klabu ya Manchester United mpaka sasa imefanikiwa kushinda michezo yake saba ambayo imecheza kwenye michuano yote.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa