Ten Hag: Wachezaji Wananisapoti

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema wachezaji wa klabu hiyo wanamsapoti na wapo nyuma yake na sio kama ambavyo inaelezwa wachezaji hawamkubali tena.

Kocha Ten Hag akiongea na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kesho dhidi ya Chelsea ameweka wazi kua hakuna tatizo lolote baina yake na wachezaji wa klabu hiyo.ten hagKumekua na uvumi ambao unaendelea kusambaa kua kocha huyo amepoteza nguvu ya ushawishi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo klabuni hapo jambo ambalo kocha huyo amekanusha.

Kocha huyo ametoa mifano kwenye michezo kadhaa ambayo inaonesha wachezjai wanampambania na wako nyuma na michezo hiyo ni dhidi ya Brentford, Fulham,na Burnley na kusisitiza kua umoja upo ndani ya timu.ten hagKlabu ya Manchester United inaelezwa kuchukua hatua kwa vyombo vya habari ambavyo vimekua vikiripoti habari za kuleta taharuki kwa klabu hiyo, Jambo ambalo limekua likimkwaza pia kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag.

Acha ujumbe