Ten Hag Yupo Kikaangoni

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag anaelezwa yupo kwenye kikaango ndani ya klabu hiyo kutokana na mwendendo wa timu hiyo kwasasa.

Ten Hag ambaye anaiongoza klabu ya Manchester United kwa msimu wa pili huu inaonekana mwenendo wa klabu hiyo mpaka sasa hauridhishi, Lakini pia ikielezwa wachezaji waandamizi klabuni hapo hawaridhishwi na mbinu za mwalimu huyo.ten hagTaarifa kutoka ndani ya klabu ya Man United zinaeleza kuna kundi kubwa la wachezaji ambalo ni karibia asilimia 50 ambalo halielewi mbinu za kocha huyo, Huku wakiamini mbinu zake hazibadiliki na hazileti matokeo ndani ya timu hiyo.

Kutokana na taarifa hiyo ni wazi kua kocha huyo anaweza kuondolewa ndani ya timu hiyo kwani wachezaji wameanza kulalamikia mbinu zake, Lakini pia wachezaji wanaelezwa pia kuchoshwa na mazoezi ya mwalimu huyo haswa kukimbia na wanadai hawajui wanakimbia kwanini.ten hagKocha Ten Hag anaweza kupitia ambacho wamepitia makocha wengine waliofukuzwa klabuni hapo kama Jose Mourinho, Louis Van Gaal, David Moyes, pamoja na Ole Gunnar Solskjaer ambao waliondolewa ndani ya timu hiyo baada ya kupishana na wachezaji kwenye timu hiyo.

Acha ujumbe