Kocha wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uholanzi Erik Ten Hag inaelezwa bado ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo zaidi licha ya matokeo yasiyo ya kuridhisha hivi karibuni.
Erik Ten Hag amekua na wakati mbaya msimu huu ndani ya kikosi cha Manchester United haswa msimu ukiwa unaelekea ukingoni, Huku matokeo yameonekana sio ya kuvutia wakiwa wamepoteza michezo 17 mpaka wakati huu ikiwa ni rekodi mpya baada ya miaka mingi kupita.Inaelezwa mmiliki mpya wa klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe anavutiwa na kocha huyo wa kimataifa wa Uholanzi akiamini ni mtu sahihi ambaye anaweza kurudisha zile zama bora kabisa za klabu ya Manchester United.
Inaripotiwa kumekua na vikao kadhaa baina ya kocha Erik Ten Hag na Bosi Sir Jim Ratcliffe pamoja na mshauri wa karibu bosi huyo Dave Braislford wakijadili ni namna gani klabu hiyo inaweza kufanya vizuri zaidi kuelekea misimu ijayo.Kumekua na tetesi mbalimbali kua huenda Manchester United ikaachana na kocha wake huyo mwishoni mwa msimu huu, Lakini mambo yanavyoendelea na ukaribu uliopo baina ya kocha huyo na bosi wa klabu hiyo inaonekana kwa kiwango kikubwa bado wana imani nae na ataendelea kuwepo klabuni hapo zaidi.