Ten Hag Yupo United Mpaka 2026

Klabu ya Manchester United hatimae imefanikiwa kumuongeza kandarasi kocha wake raia wa kimataifa wa Uholanzi Erik Ten Hag ambaye ataendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2026.

Mkataba wa kocha Erik Ten Hag ulikua unamalizika mwaka 2025 hivo kwa maana hiyo ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwepo ndani ya viunga vya Old Trafford, Hii ikiwa na maana kua kocha huyo wa kimataifa wa Uholanzi anapewa nafasi nyingine ya kuonesha kwanini mabosi wa klabu hiyo wamemuamini.ten hagTaarifa za awali zilikua zikieleza kua kocha huyo huenda akatimuliwa ndani ya Man United baada ya msimu jana kumalizika kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo, Lakini klabu hiyo haikufanya hivo na badala yake imeamua kumuamini na kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja ili kuendelea kuijenga United mpya ambayo itarejesha utawala wake kama ilivyokua hapo kabla.

Mkurugenzi wa ufundi mpya wa klabu ya Manchester United Dan Ashworth ameweka wazi kua wana imani na kocha wao na ni moja ya makocha waliofanikiwa kwenye bara la ulaya kwa misimu miwili iliyopita baada ya kutwaa taji katika kila msimu ambao amefundisha klabu hiyo.ten hagKocha Erik Ten Hag yeye anasema anayaona maendeleo ndani ya timu tofauti na alivyoikuta na ana matumaini makubwa ya kuendelea kufanya vizuri na kuirudisha Man United inapostahili, Kwani mpaka sasa anahesabika kama kocha aliyefanikiwa zaidi ndani ya timu hiyo kwa misimu ya hivi karibuni akitwaa mataji mawili mpaka sasa.

Acha ujumbe