Bianca Andreescu alipokelewa kwa shangwe kwenye Canadian Open, lakini safari yake jijini Toronto haikudumu kwa muda mrefu. Akipewa wildcard ya kushiriki mashindano ya nyumbani, bingwa wa US Open 2019 alifungwa 5-7, 4-6 na Nikola Bartunkova katika mechi ya ufunguzi. Pia alishiriki doubles na Kayla Cross, lakini wakapoteza dhidi ya Ulrikke Eikeri na Quinn Gleason.

Licha ya matokeo hayo, Andreescu alionyesha furaha kubwa kwa mashabiki wake. Kupitia Instagram, aliandika, “Toronto, siku zote mnanikumbusha kwanini nafanya hivi, kucheza nikiwa nyumbani, hisia za sapoti yenu na kuwaona watu wengi ninaowafahamu wakiwa jukwaani, hii ina maana zaidi ya ninavyoweza kueleza.” Ujumbe wake wa hisia ulionyesha shukrani kwa mashabiki waliompa nguvu katika kila hatua ya safari yake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Sasa macho yake yameelekezwa kwenye michuano ya Cincinnati Open, ambapo ataanza safari ya kufuzu dhidi ya Wang Xiyu. Hii ni nafasi ya kujaribu kuandika sura mpya baada ya ukame wa mataji msimu huu. Mashabiki wanatazamia kuona kama anaweza kurudia maajabu ya 2019, aliposhinda Indian Wells, Toronto na US Open akiwa na umri wa miaka 19 pekee.
Ushindi wake wa kihistoria dhidi ya Serena Williams kwenye fainali ya US Open 2019 (6-3, 7-5) uliweka jina lake kwenye vitabu vya rekodi. Andreescu alikua mchezaji wa kwanza kushinda US Open kwenye ushiriki wa main-draw, na pia Mkanada wa kwanza kutwaa taji kubwa la singles.

Kwa sasa, Andreescu anabaki kama mfano wa uvumilivu na mapenzi ya nyumbani. Toronto imemkumbusha kwa nini anapenda mchezo huu, na Cincinnati inaweza kuwa jukwaa la kuonyesha kwamba safari yake bado ina nguvu na matumaini.


