Katika hali isiyo ya kawaida, aliyewahi kuwa mchezaji namba 1 kwa ubora kwenye mchezo wa tenesi – Andy Murray, hakushangazwa na Novak Djokovic kutwaa ubingwa wa Australian Open.
Djokovic alifanikiwa kutwaa ubingwa wa 18 wa Grand Slam kwenye fainali ya Australian Open 2021 baada ya kumzidi ufundi Daniil Medvedev kwenye seti zote.
Murray anasema ni kama tu hakufatilia kabisa mashindano ya mwaka huu ambapo alilazimika kutoshiriki baada ya kukubwa na maambukizi ya COVID 19.
“Niliangalia kidogo sana, nilitaka kushiriki lakini ilikuwa ngumu. Niliacha kuwafatilia wachezaji wote wa tenesi ambao nilikuwa ninawafatilia kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu sikutaka kuangalia kinachoendelea.” Alisema Andy Murray.

Murray alitegemea Medvedev angekuwa na upinzani mkubwa kwa Djokovic lakini hata yeye alifahamu namna ilivyongumu kupambana na bingwa huyu wa dunia kwenye fainali ya Grand Slam.
“Ni sehemu tofauti sana kurudi au kucheza kwenye fainali ya Grand Slam, kuliko kwenye robo au nusu fainali hasa unapokutana na mtu ambaye ameshashinda mara 17.
“Inaogopesha lakini wachezaji chipukizi nao wameonesha jinsi gani wapo mbali katika kufikia nafasi hizi. Kwenye US Open, Dominic Thiem alifanya kile alichotakiwa kukifanya ili ashinde. Lakini kama Novak hakumpiga mwamuzi na mpira kwenye koo, ninadhani yangekuwa ni matokeo kama haya”
TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET
BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.
Novak yupo vinzur
Habari njema
Novak namuelewa
Vizuri
Jamaa anajua sanaa
Djokovic hakupata wapinzani wa kweli kama Andy na Nadal. Alikutana na chipukizi wengi
Safi
Nice
Nice
kwa kweli