Baada ya kukaa nje ya uwanja toka mwezi Machi, aliyewahi kuwa mchezaji namba moja (kwa wanaume) duniani, Andy Murray anatarajia kuanza kujifua wikiendi hii.

Murray atasafiri kuelekea Rome-Italia ambapo anatarajia kuanza kujiimarisha zaidi kwa michezo ya mazoezi dhidi ya baadhi ya wachezaji nyota watakaoshiriki mashindano ya Italian Open 2021.

Miongoni mwa wachezaji atakaojifua nao ni Novak Djokovic na Diego Schwartzman. Andy Murray alikuwa nje ya uwanja baada ya kujiondoa kwenye Miami Open kutokana na majeruhi na baadae aligundulika kupata maambukizi ya COVID19 na hivyo akaendelea kuwa nje kwa muda.

“Ninataka kuwa karibu na wachezaji wakubwa kwenye mashindano makubwa. Jumapili nimepangiwa kuanza na Diego Schwartzman na kisha mchana nitacheza na Novak.

“Ninataka kuchuana na wachezaji wenye viwango vikubwa kadiri inavyowezekana kwa sababu nadhani hiyo itanisaidia kurejea kwenye kiwango changu haraka zaidi.” Alisema Murray

Pamoja na yote, Murray anaimani atapatiwa nafasi ya kucheza mashindano ya French Open 2021 ambayo yataanza Mei 30 licha ya kuwa, shirikisho la mchezo wa tenesi nchini Ufaransa, linataka kumuona Andy Murray akiwa uwanjani kabla ya kufanya uamuzi wa kumruhusu kushiriki mashindano hayo.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Andy Murray, Andy Murray Kujifua na Novak Djokovic., Meridianbet

SOMA ZAIDI

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa