Katika michuano ya National Bank Open usiku wa Jana, Ben Shelton alionyesha kiwango cha juu ambacho wachache wangeweza kuhimili. Bingwa mtetezi huyo aliingia nusu fainali bila kupoteza seti, akimshinda Jakub Mensik kwa kishindo 6-3, 6-1.

Takwimu zake zilikuwa za kuvutia, ushindi mara 18, makosa matatu pekee, na 89% ya pointi za first serve kushinda. Hakukabiliwa na break point hata moja na alitoa serve ya kasi ya 147 mph. Shelton alisema, “Nilihisi vizuri sana. Nilifurahia sana mchezo wangu wa kurudisha. Nadhani kiwango nilichokidumisha kilikuwa cha juu sana.”
Ben Shelton anasimama katika michuano hii kama bingwa mtetezi, akitafuta kutwaa taji mfululizo Montreal, huku mshindani wake Jakub Mensik akiwa mchezaji mwenye rekodi ya kuvutia dhidi ya Top 10, lakini alishindwa kabisa na Shelton.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Ben Shelton alionyesha ustahimilivu na ubunifu, mfululizo wa mashuti 24 kwenye pointi ya pili ya mechi, forehand kali, na backhand returns zilizokua ngumu kuimili. Mensik, aliyewahi kumshinda mara mbili, hakuwa na majibu.

Ben Shelton aliandika kwenye kamera baada ya mechi, “sijamaliza.” Kauli inayosisitiza kwamba safari yake Montreal bado inaendelea. Mshindi kati ya Learner Tien na Daniel Merida ndiye atakayekutana naye kwenye nusu fainali.

