Mashindano ya ATP Finals 2020 yamemalizika na Daniil Medvedev ameumaliza mwendo kwa kubeba taji kubwa zaidi kwenye maisha yake ya uchezaji tenesi mpaka sasa.
Fainali ya ATP 2020 ilimkutanisha Medvedev dhidi ya Bingwa wa US Open 2020 – Dominic Thiem katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa O2 Arena jijini London – Uingereza.
Daniil Medvedev ameshinda mchezo wa fainali kwa matokeo ya seti 4-6 7-6 (7-2) 6-4. Licha ya Thiem kuongoza kwenye seti ya 2, Medvedev alipambana kuzitafuta pointi 7 katika seti ambayo ilipelekea kuchezwa seti ya ziada ili kumpata mshindi.
Ubingwa wa ATP Finals 2020, unamfanya Daniil Medvedev kumaliza mwaka akiwa nafasi ya 4 kwa ubora duniani.
Medvedev anakuwa mchezaji wa kwanza kuwafunga wachezaji watatu bora duniani katika shindano moja. Aliwafunga Novak Djokovic na Rafael Nadal. Hakuwa amemfunga mchezaji yeyote aliyepo kwenye 10 bora tangu November 2019 mpaka Oktoba 2020, sasa amewafunga wachezaji 7 ndani ya wiki 4.
Mashindano ya ATP Finals yamefanyika Uingereza kwa mara ya mwisho, kuanzia 2021 mashindano hayo yatakuwa yakifanyika jijini Turin – Italia.
Hadi 130,000,000 Tsh kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.




Mwajumah
Hongera sana Daniil
angelina
goodupdate
Shakila mrope
Safi san
Tatu
Saginaw sana
Tatu
Safi sana
magdalena
pongezi kwake
Adelta
Congar medvedved👏👏
Povel
Congratulations kwake
Sauda
Safi sana
samiah
Safi
Zainabu kihongosi
Good
warda
Hongera yake