Djokovic Aianza Safari Ya Melbourne Kibabe

Novak Djokovic amefungua rasmi safari yake ya kutafuta taji la 11 la Australian Open na Grand Slam ya 25 kwa mtindo wa kuvutia jijini Melbourne. Mserbia huyo namba nne Duniani alionyesha ubora mkubwa tangu mwanzo, akithibitisha kuwa bado ana kiu kubwa ya kuandika historia mpya katika michuano hii.

Djokovic alimshinda Mhispania Pedro Martinez kwa seti tatu za moja kwa moja 6-3, 6-2, 6-2 kwenye uwanja wa Rod Laver Arena, katika mchezo uliodhibitiwa kikamilifu. Akiwa na mchezo bora sana, Djokovic alipoteza pointi tatu tu kwenye mechi nzima, takwimu inayoonyesha wazi namna alivyokuwa juu kiufundi na kimbinu dhidi ya mpinzani wake aliye nafasi ya 71 Duniani.

Djokovic Aianza Safari Ya Melbourne Kibabe

Ushindi huo haukuwa wa kawaida, kwani ulimfanya Djokovic kufikisha ushindi wake wa 100 katika historia ya Australian Open, hatua ambayo haijafikiwa na mchezaji mwingine yeyote. Djokovic amesema kufikia rekodi hiyo ni jambo la kujivunia, akieleza kuwa kuvunja rekodi na kuendelea kuweka historia kumekuwa motisha kubwa kwake.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo, Djokovic alisema Rod Laver Arena ni uwanja anaoupenda zaidi kutokana na kumbukumbu nyingi nzuri alizopata hapo kwa zaidi ya miaka 20. Ameahidi kuendelea kutoa kiwango cha juu kama njia ya kurudisha shukrani kwa mashabiki waliomuunga mkono, akisisitiza kuwa bado anajisikia mwenye nguvu kucheza katika kiwango cha juu.

Djokovic Aianza Safari Ya Melbourne Kibabe

Kwa kucheza mchezo huo, sasa amelingana na Roger Federer kwa rekodi ya kushiriki Australian Open mara 21 na Grand Slam kwa ujumla mara 81. Sasa macho yataelekezwa kwenye raundi ya pili, ambapo atakutana na Muitaliano Francesco Maestrelli.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.