Novak Djokovic anaingia kwenye hatua ya mwisho ya msimu wa 2026 akiwa na lengo moja kubwa, kutwaa taji la 25 la Grand Slam na kuvunja rekodi ya kihistoria. Baada ya kushinda US Open mwaka 2023 na kufikisha mataji 24, amekuwa akikaribia mara kadhaa lakini akakosa. Mwaka huu, alifika fainali ya Australian Open kabla ya kuzuiwa na Carlos Alcaraz, akatolewa raundi ya tatu Roland Garros, na akafika nusu fainali Wimbledon akapigwa na Jannik Sinner.

Sasa US Open ndiyo nafasi yake ya mwisho msimu huu. Lakini ratiba yake imezua mjadala. Djokovic amethibitisha atashiriki Cincinnati Open kwa mara ya kwanza tangu 2023, wiki moja tu kabla ya US Open kuanza. Hii inaweza kumchosha kimwili, hasa ikizingatiwa changamoto zake za stamina kwenye mashindano makubwa miaka ya hivi karibuni.
Mara ya mwisho alicheza Cincinnati 2023, alishinda kwa kishindo dhidi ya Alcaraz kwenye fainali ya kusisimua na kisha akatwaa US Open. Lakini sasa akiwa na miaka 39, hali ya mwili wake ni tofauti. Mashabiki wanajiuliza kama kurudi Cincinnati ni sehemu ya maandalizi au kosa litakalomgharimu nafasi ya historia.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kipengele kingine cha kusisimua ni kwamba Djokovic hatashiriki tu singles, bali pia mixed doubles akishirikiana na Aryna Sabalenka. Hii ni mara ya kwanza kwa muda mrefu kujaribu mashindano mawili kwa wakati mmoja. Ratiba inamaanisha kwamba kama atafika fainali Cincinnati Agosti 23, atakuwa na siku moja pekee ya kupumzika kabla ya kuanza US Open na pia kuingia kwenye mashindano ya mchanganyiko tarehe 25.

Kwa sasa, hali ya Alcaraz haiko sawa kiafya, jambo linaloweza kumpa Djokovic faida kidogo. Lakini kwa kujiingiza Cincinnati, huenda ameifuta faida hiyo mwenyewe. US Open 2026 inakuja kama jukwaa la mwisho la kuandika historia kwa Djokovic kama ataongeza taji la 25 na kujiweka juu ya rekodi zote.



