Mashindano ya Western and Southern Open yanaendelea kutimua vumbi mjini Cincinnati – Marekani. Novak Djokovic na Johanna Konta wanaendelea kuwaburuza wapinzani wao na sasa wamefuzu hatua ya nusu fainali.
Katika michezo yao ya robo fainali, Novak alikutana na Jan-Lennard Struff wakati Konta alichuana na Maria Sakkari.
Djokovic na Konta waendeleza ubabe kwenye michuano ya Western na Southern Open.
Katika mchezo uliokuwa wa waina yake, Novak alimgaragaza Mjerumani – Jan Lennard Struff kwa seti 6-3 6-1 na kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo katika michezo 21 aliyoicheza mwaka huu.

“kiujumla nimefurahi, nilikuwa ninacheza vizuri na nimepiga mipira vizuri na kujipatia pointi.” amesema bingwa wa Australian Open na Wimbledon – Novak Djokovic.
Johanna Konta alikuwa na wakati mzuri baada ya kumgaraza kirahisi Maria Sakkari ambaye alimtoa Serena Williams. Konta aliibuka na ushindi wa seti 6-4 6-3 na hivyo amefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Akiwa kwenye kiwango bora tangu kuanza kwa Mashindano haya, Konta amesema “Nilifurahi kwa kuweza kuumudu mchezo na kuwa mgumu kila nilipohitahika kuwa hivyo. Niliweza kushindana kwa baadhi ya sehemu za mchezo ambazo niliziona ni muhimu wakati tunacheza.”

Kufuatia kuibuka kwa maandamano yanayopinga mauaji ya watu weusi baada ya mauaji ya Jacob Blake aliyeshambuliwa kwa risasi na polisi, michezo mingi nchini Marekani imesimama kwa muda.
Shirikisho la mchezo wa tenisi nchini humo – US Tennis Association, ATP na WTA wamesema, “mchezo wa tenis kwa pamoja unapinga vitendo vya ubaguzi wa rangi na uvunjwaji wa haki za binadamu.”
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


Zeiyana
Kila kitu kinaenda na wakati kwa sasa wakati wa Serena kutamba kwenye tens ushakwisha
Caroline
Hongera zao
Lydia Emmanuel Magoti
Mambo mazuri kwa Djokovic kutesa kwazamu Sasa wakina Selena wakae Chini sasa
farida ahmadi
Pongezi Sana kwao
Mwanahamisi
Hongera zao
Shan
Well done!
rama
safii sana yani
Sauda
Pongezi kwao
Dorophina
Hongera kwao da nilijua Serena atawakilisha kama kawaida
aisha
Big up kwao
Mwajumah
Pongezi kwao#Meridianbetz
Ester jackson
Habari njema
Furahav
Vizuri
Sabrina
Inapendeza sana
Theonestina
Hongera zao
jullie
hongera sana
David Pere
kiujumla nimefurahi, nilikuwa ninacheza vizuri na nimepiga mipira vizuri na kujipatia pointi.” amesema bingwa wa Australian Open na Wimbledon – Novak Djokovic.
Janeflora malisa
Nice
Nasra
Gud
magdalena
habari njema hizi na pongezi kwao
warda
Hongera yao
felister
hongera yao jamani
Tatu
Pongezi kwao
Shafii
Hii ni habari njema kwa wana tenis inavuta.
Antony Luseno
Djokovic katisha sana
lombo
saf
Rose kapinga
Pongezi kwao wako vizuri!!!
neema hassan
Pongezi kwao
Asia Abdy
Nice
Samiah
Gud
Samira
Wapo vizuri sana pongezi nyingi kwao