Bingwa wa US Open – Dominic Thiem, amechukua uamuzi wa kujitoa kwenye mashindano ya Wimbledon baada ya kupata majeruhi.
Mashindano ya Wimbledon yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi jumatatu ijayo na yatadumu mpaka Julai 11, 2021. Kujiondoa kwa Thiem ni matokeo ya mchezaji huyo kuumia kiuno kwenye mchezo dhidi ya Adrian Mannarino Jumanne hii

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dominic Thiem ameandika ” nitafanya kila nilichoambiwa na madaktari ili nirejee kwenye hali yangu mapema iwezekanavyo.
“Nitajitahidi kurejea uwanjani mapema kadiri niwezavyo” . Kabla ya kujitoa kwenye Wimbledon, Thiem alijitoa kwenye mashindano ya Olympics ili ajiweke imara kwa mashindano ya Wimbledon sambamba na kutetea ubingwa wake wa US Open mwaka huu.