Kuelekea mashindano ya French Open 2021, mchezaji namba 3 kwa ubora duniani (kwa wanawake) kunako mchezo wa tenesi – Simona Halep, amejiweka kando kwa sasa.
Halep anakaa pembeni kutokana na kupata majeruhi ambayo yatamuhitaji kutumia muda mrefu ili kujiweka sawa. Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea mashindano ya French Open ambayo yamepangwa kuanza Mei 20,2021 , Halep anaamini muda sio rafiki kwake katika kuhakikisha anashiriki mashindano hayo.
Halep atayakosa mashindano haya ambayo ameshacheza fainali 3 na mwaka 2019 alibeba taji la Wimbledon. Endapo kama atakuwa vizuri kiafya, Juni 28, 2021 ataingia kwenye mashindano hayo (Wimbledon Open) akiwa kama bingwa mtetezi.
2018 alibeba taji la Rolland Garros baada ya kumfunga Sloane Stephens kwenye mchezo wa fainali. Mwaka jana alifika hatua ya mzunguko wa 4 na alitolewa na bingwa mtetezi , Swiatek.
Majeruhi yameendelea kuwa kikwazo, kwenye Italian Open, Ashleigh Barty amejiondoa kwenye hatua ya robo fainali baada ya kupata majeruhi akiwa mchezoni.
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.
Magdalena
Pole Sana kwake ndo changamoto za mchezo
Shakila
Pole yake
Sauda
Pole sana