Hayawi hayawi sasa yamekuwa, fainali ya mashindano ya French Open 2021 kuwakutanisha wachezaji wawili ambao pengine hawakupewa nafasi ya ushindi mwaka huu.

Barbora Krejcikova uso kwa uso na Anastasia Pavlyuchenkova. Krejcikova anatinga hatua ya fainali kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake ya mchezo wa tenesi. Hii ni hatua kubwa kwa Krejcikova kama ilivyo kwa Pavlyuchenkova ambaye pia ni mara ya kwanza anacheza fainali ya Grand Slams.

French Open 2021, French Open 2021, Krejcikova vs Pavlyuchenkova, Meridianbet
Barbora Krejcikova

Krejcikova alichuana na Maria Sakkari kwenye mchezo wa nusu fainali ya French Open 2021. Baada ya mtanange mkali uliodumu kwa takribani masaa 3, Krejcikova aliibuka kidedea kwa matokeo ya seti 7-5 4-6 9-7.

Upande wa pili, Pavlyuchenkova alikuwa akichuana na  Tamara Zidansek kwenye mchezo wa nusu fainali ya mashinano haya. Matokeo ya seti 7-5 6-3 yalitosha kumvusha Pavlyuchenkova na sasa atacheza fainali yake ya kwanza ya Grand Slams.

French Open 2021, French Open 2021, Krejcikova vs Pavlyuchenkova, Meridianbet
Anastasia Pavlyuchenkova

Nani kuibuka kidedea kwenye mashindano ya Roland Garros msimu huu, ni Krejcikova au Pavlyuchenkova? Jumamosi hii itatoa majibu sahihi.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa