French Open 2021 Kughairishwa.

Hali sio shwari nchini Ufaransa kufuatia ongezeko la visa vya COVID-19. Mashindano ya French Open 2021, hatarini kughairishwa.

Taarifa hii inatokana na tamko la waziri wa Michezo wa Ufaransa, Roxana Maracineanu.

Ufaransa wameingia kwenye “lockdown” kwa Mara ya tatu Jumamosi wiki iliyopita na raisi wa nchi hiyo, Emmanuel Macron anategemea utaratibu huo utaisha katikati ya mwezi Mei.

Mashindano ya French Open, yalipangwa kuanza Mei 23-Juni 6, 2021 katika viwanja vya Roland Garros. 2020 mashindano haya yalighairishwa kutokana na wimbi kubwa la maambukizi ya COVID-19.
French Open
swiatek alibeba taji la French open kwa Mara ya kwanza 2020

“Tupo kwenye majadiliano na Shirikisho la Tenisi la Ufaransa ili kuona kama tunaweza kubadilisha tarehe iendane na uwezekano wa kurejesha Michezo na matamasha yote makubwa.

“Leo, japo kuwa baadhi ya Michezo inaendelea, tunajaribu kupunguza hatari ya kuenea kwa virusi kwenye sekta ya michezo” Maracineanu aliiambia radio France Info.

Ufaransa inapambana na uwepo wa wagonjwa 5,000 waliopo chini ya uangalizi maalumu. Mpaka kufikia ijumaa (wiki iliyopita), nchi hiyo ilirekodi visa 46,677 na vifo 304 vitokanavyo na COVID-19.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

5 Komentara

    French kumenogaaa

    Jibu

    Ni Bora waairishe tu hili gojwa lituliye kidogo

    Jibu

    Gonjwa limepamba moto ni sawa tu waarishe

    Jibu

    Hili gonjwa inabidi tulizoee kama marelia

    Jibu

    Duh

    Jibu

Acha ujumbe