Utamu wa mashindano ya French Open 2021 upande wa wanaume, sasa ndio unaanza. Huku Rafael Nadal vs Novak Djokovic, kule Stefano Tsitsipas vs Alexander Zverev.

Baada ya kupita kwenye kila hatua tangu kuanza kwa mashindano ya Roland Garros 2021, sasa tunaingia hatua ya nusu fainali kwa upande wa wanaume. Nani kufuzu hatua ya fainali na pengine kuibuka kidedea mwaka huu?

Macho ya wengi yapo kwenye mchezo utamkutanisha Rafael Nadal vs Novak Djokovic. Hapa tunawaongelea wachezaji wakongwe na bora zaidi upande wa wanaume. Mchezo huu utamkutanisha bingwa mtetezi (Nadal) dhidi ya mchezaji wa kwanza kwa ubora duniani kwa sasa.

French Open 2021, French Open 2021, Nadal vs Djokovic X57., Meridianbet
Djokovic (kushoto) vs Nadal (kulia)

Ni dhahiri kuwa Nadal ndiye mtawala wa mashindano ya French Open akiwa na jumla ya mataji 13 akilinganishwa na Djokovic (taji 1). Japokuwa, kwa ujumla Djokovic anamataji mengi ya Grand Slams (29) akilinganishwa na Nadal (28). Nadal vs Djokovic ni mchezo ambao umeshachezwa kwa mara 57 na sasa watakutana tena leo kwa mara ya 58.

Mchezo mwingine wa nusu fainali ya French Open 2021 utamkutanisha Stefano Tsitsipas vs Alexander Zverev. Huu ni mchezo ambao utawakutanisha wachezaji wawili wanaoendana kwa kiasi fulani.

French Open 2021, French Open 2021, Nadal vs Djokovic X57., Meridianbet
Tsitsipas (kushoto) vs Zverev (kulia)

Ukizungumzia fainali za Grand Slams, Tsistipas hajawahi kucheza fainali lakini Zverev amecheza fainali 1. Kama ni mataji ya ATP, kabatini kwa Tsitsipas yapo 7 huku kwa Zverev yakiwa mataji 15.

Tsitsipas na Zverev wameshakutana mara 7 huku Tsitsipas akishinda mara 5 na Zverev mara 2. Nani kumzidi kete mwenzake kwenye mchezo wa nusu fainali?

Mshindi kati ya Nadal vs Djokovic na Tsitsipas vs Zverev watachuana kwenye fainali ya French Open 2021 jumapili hii!


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa