Hatimaye mashindano ya French Open 2021 kufikia tamati wikiendi hii. Upande wa wanaume, Novak Djokovic atachuana na Stefano Tsitsipas kwenye fainali.

Djokovic alikuwa uwanjani kuchuana na mpinzani wake wa muda wote, Rafael  Nadal kwenye mchezo wa nusu fainali. Licha ya kuanza vibaya mchezo, Djokovic alifanikiwa kurejea uwanjani na kutumia nafasi za makosa ya Nadal kumuadhibu vilivyo!

french open 2021, French Open 2021 Ni Djokovic vs Tsistipas, Meridianbet

Nadal anashika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wacheza tenesi wenye mataji mengi ya French Open (13) akilinganishwa na Djokovic (1), safari yake ya kuwania taji la 14 imetishwa kwa matokeo ya seti 3-6 6-3 7-6 (7-4) 6-2 katika mchezo uliochezwa kwa takribani masaa manne.

Sambamba na ushindi wa Djokovic, nyota huyu ameongeza wigo wa michezo aliyoshinda dhidi ya Nadal na sasa ni michezo 30 kati ya 58 waliyokutana kwenye maisha yao ya mchezo wa tenesi.

french open 2021, French Open 2021 Ni Djokovic vs Tsistipas, Meridianbet

Upande wa pili kunako nusu fainali ya French Open 2021, Stefano Tsitsipas amefanikiwa kumuondoa Alexander Zverev kwenye mashindano haya baada ya kumshinda kwa seti 6-3 6-3 4-6 4-6 6-3.

Ushindi wa Tsitsipas dhidi ya Zverev, unamfanya mchezaji huyo kuwa mgiriki wa kwanza kucheza fainali ya mashindano ya Grand Slam. Fainali ya French Open 2021(kwa wanaume) itachezwa Jumapili hii.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa