Gauff Akabiliwa na Mtihani Mkubwa wa Uwanja Wa Nyasi

Coco Gauff anaendelea kutafuta mwanga kwenye msimu wa nyasi baada ya kuanza vibaya maandalizi ya Wimbledon kufuatia kipigo kutoka kwa Paula Badosa kwenye Berlin Open. Nyota huyo wa Marekani, ambaye alipata muda zaidi wa kujiandaa baada ya kutolewa mapema Roland Garros mwaka huu, bado hajashinda mchezo wowote wa singles kwenye nyasi tangu mwaka 2024.

Gauff Akabiliwa na Mtihani Mkubwa wa Uwanja Wa Nyasi

Aliyekuwa namba moja duniani katika mchezo wa doubles, Rennae Stubbs, ameeleza kuwa matatizo ya Gauff kwenye nyasi yanatokana zaidi na namna anavyopiga forehand yake. Kwa mujibu wa Stubbs, matumizi ya Western grip yenye mwinuko mkubwa si rafiki kwa viwanja vya nyasi vinavyohitaji mipira ya kasi na mapigo ya moja kwa moja.

Mbali na forehand, Stubbs pia ameonyesha kuwa save ya pili ya Gauff ni eneo jingine ambalo wapinzani wake huweza kulishambulia kirahisi. Anaamini kuwa udhaifu huo huonekana zaidi kwenye nyasi kuliko kwenye viwanja vya udongo au hard court. Kwa maoni yake, Gauff anahitaji kubadilisha mbinu zake kwa kutegemea zaidi backhand yake na kujaribu kwenda mbele karibu na neti mara nyingi zaidi.

Gauff Akabiliwa na Mtihani Mkubwa wa Uwanja Wa Nyasi

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Licha ya changamoto hizo, Gauff bado ni mmoja wa nyota wenye matumaini makubwa kwenye tenisi ya wanawake. Akiwa na miaka 22, atakuwa akicheza Wimbledon kwa mara ya saba mfululizo. Alijitangaza duniani mwaka 2019 alipomshangaza Venus Williams akiwa na miaka 15 pekee, lakini tangu wakati huo hajawahi kuvuka hatua ya raundi ya nne kwenye michuano hiyo.

Gauff Akabiliwa na Mtihani Mkubwa wa Uwanja Wa Nyasi

Wimbledon imebaki kuwa Grand Slam yenye rekodi ngumu zaidi kwa Gauff. Mwaka jana alitolewa mapema na Dayana Yastremska, na ushindi wake wa mwisho kwenye nyasi ulitokea Wimbledon 2024 dhidi ya Sonay Kartal. Huku michuano ya mwaka huu ikitarajiwa kuanza Juni 29, Gauff atakuwa na dhamira ya kuvunja ukame huo na kuthibitisha kuwa bado anaweza kung’ara hata kwenye uso ambao umekuwa ukimpa changamoto kubwa zaidi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.