Katika muendelezo wa mashindano ya Italian Open 2021, Rafael Nadal na Novak Djokovic wametinga hatua ya robo fainali baada ya kufanikiwa kupindua matokeo.

Nadal alikuwa uwanjani akichuana na Denis Shapovalov. Licha ya Nadal kupoteza pointi kwenye seti ya awali, alirejea mchezoni na kupindua meza katika seti zilizofuata.

Matokeo ya seti  3-6 6-4 7-6 (7-3), yalimtosha Nadal kumgaragaza Shapovalov katika mtanange uliotumia takribani masaa 3 na nusu. Rafael Nadal anashiriki mashindano haya akiwa na lengo la kuusaka ubingwa wa 10 wa Italian Open.

Upande wa pili, kwa mara ya 15 mfululizo, Novak Djokovic ametua hatua ya robo fainali ya mashindano haya. Kama ilivyokuwa kwa Nadal, mchezaji namba 1 kwa ubora duniani (wanaume) na bingwa mtetezi, Djokovic alipindua matokeo dhidi ya Alejandro Davidovich Fokina na kushinda kwa seti 6-2 6-1.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Italian Open, Italian Open: Nadal na Djokovic Watua Robo Fainali., Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa