Katika hali ambayo haikutegemewa na wengi, Serena Williams, Naomi Osaka na Simona Halep wote wameyaaga mashindano ya Italian Open 2021.

Williams alirejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari lakini amejikuta akipoteza mchezo wake wa 1000 akiwa kama mchezaji nguli wa tenesi.

Williams alikuwa uwanjani akichuana na Nadia Podoroska ambaye alimbwaga bingwa huyu wa Grand Slams mara 23 kwa seti 7-6 (8-6) 7-5. Ushindi dhidi ya Serena Williams, unampatia nafasi Podoroska kufuzu hatua ya 16 bora kunako mashindano ya Italian Open.

Italian Open
Serena William

Naomi Osaka ameendelea kuwa na matokeo mabaya kwenye viwanja vya tope. Kwa mara ya pili, Mjapani huyu amejikuta akiambulia kipigo cha seti 7-6 (7-2) 6-2 kutoka kwa Jessica Pegula. Huu ni mwanzo mbaya kwa Osaka ambaye anajiandaa na mashindano ya French Open yanayotarajiwa kuanza Mei 30,2021.

Simona Halep alijikuta akilazimika kutoka uwanjani baada ya kupata majeruhi wakati akichuana na Angelique Kerber. Mpaka Halep anatoka uwanjani, tayari alikuwa anaongoza kwa matokeo ya seti 6-1 3-3 na punde ataanza matibabu ya majeraha yake.

Italian Open, Italian Open: Williams na Osaka Watolewa Nje., Meridianbet
Halep akitoka uwanjani baada ya kupata majeruhi.

Muendelezo wa Italian Open ulikuwa ni furaha kwa Ashleigh Barty baada ya kufuzu mzunguko wa tatu kwa kumfunga Yaroslava Shvedova kwa seti 6-4 6-1.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Italian Open, Italian Open: Williams na Osaka Watolewa Nje., Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa