Miami Open: Medvedev Afuzu, Norrie Atolewa.

Mambo yanazidi kunoga kwenye mchezo wa tenesi. Safari hii tunaangazia mashindano ya Miami Open 2021. Mzunguko wa tatu umekuwa na matokeo ya aina yake, wengine wanafuzu huku wengine wakifungasha virago na kuambiwa asanteni kwa kushiriki.

Imekuwa hivyo kwenye mchezo wa Cameroon Norrie vs Taylor Fritz upande wa pili ilikuwa ni Daniil Medvedev vs Alexei Popyrin kwenye mzunguko wa 3 wa Miami Open,2021.

Norrie alijikuta akiangukia pua licha ya kuwa mgumu mpaka mchezo wao kuamuliwa kwa seti ya ziada/ seti ya maamuzi. Matokeo ya seti 6-4 3-6 6-1, yalimtosha Mmarekani- Taylor Fritz kufuzu mzunguko unaofuata.

Norrie (kushoto) akipongezana na Fritz (kulia) baada ya mchezo wao.

Daniil Medvedev alipambana kwa kila hali licha ya kusumbuliwa na maumivu ya misuli kukaza. Licha ya kuongoza kwa matokeo ya 5-2 kwenye seti ya kwanza, mambo yalianza kumuendea kombo (Medvedev) baada ya kupata maumivu kwenye mguu wake.

Maumivu hayakumfanya Medvedev apotee mchezoni. Alijitahidi kufanikisha lengo lake na kuibuka mshindi mwishoni mwa mchezo kwa matokeo ya seti 7-6 (7-3) 6-7 (7-9) 6-4 dhidi ya mpinzani wake – Alexei Popyrin raia wa Australia.

Medvedev akiugulia maumivu ya misuli kwenye mchezo dhidi ya Popyrin

“Huenda huu ukawa ndio ushindi wangu nilioupenda zaidi. Kwa sababu, nilikuwa na maumivu makali kwenye seti ya tatu.

“Kitu pekee nilichokuwa ninakifikiria ni kutoanguka chini. Kwa sababu, kama ningeanguka chini, sidhani kama ningeweza kusimama tena.” Alisema Medvedev.

Kwa matokeo haya, Medvedev atachuana na Mmarekani – Frances Tiafoe katika kuiwania nafasi ya kucheza robo fainali ya Miami Open,2021.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Vizuri

    Jibu

    Medredev anastahili pongezi kwake

    Jibu

    Dah

    Jibu

    Hongera Medvedev

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

Acha ujumbe