Mambo yanazidi kunoga kunako mchezo wa tenesi. Mashindano ya Miami Open, 2021 yanaendelea kushika hatamu. Kushinda na kushindwa zote ni sehemu za mchezo.
Mjapan, Naomi Osaka ameendelea kuwa mwiba kwa upande wa wacheza tenesi wanawake. Katika mpambano dhidi ya Elise Mertens, Osaka alimaliza mchezo kwa matokeo ya seti 6-3 6-3 huu ukiwa ni ushindi wake wa 23 mfululizo. Osaka hajapoteza mchezo wowote ikiwa ni sambamba na kushinda fainali mbili – US Open na Australian Open 2020.

Kwingineko kwenye Miami Open 2021, mchezaji namba 1 wa Australia, Ashleigh Barty amefuzu hatua ya robo fainali kwa kumbwaga Victoria Azarenka raia wa Belarus.
Matokeo ya seti 6-1 1-6 6-2, yalimtosha Barty kumgaragaza na kumtoa nje ya mashindano Azarenka ambaye pia alicheza fainali ya US Open 2020 na kufungwa na Osaka.

Kwa matokeo haya, Osaka anaweza akachuana na Maria Sakkari (Mgiriki) au Jessica Pegula (Mmarekani) kwenye hatua ya robo fainali ya Miami Open 2021.
Barty ambaye pia anacheza mashindano ya kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani mwaka mmoja kwa sababu ya COVID19, atapambana na Aryna Sabalenka (raia wa Belarus) ikiwa ni muendelezo wa kutetea taji lake.
UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.
Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?
dorophina
Osaka yupo vizuri htr
Caroline
Safi sanaaa
Sarah
Osaka yupo vizuri
Venerose
Safi sana
Lydia Emmanuel Magoti
Osaka wapo vizuri
Hopemwaikuka
Osaka kiboko
warda
barty anajua mpaka kero