Kuelekea mashindano ya Olympics 2020, mchezaji wa tenesi namba 1 duniani (kwa wanawake), Naomi Osaka ana mashaka na uwezekano wa tukio hilo kutokea.

Kumekuwa na ongezeko la visa vya COVID19 jijini Tokyo, Japan hali ambayo inampa mashaka Osaka kama mazingira yatakuwa ni salama kwa mashindano ya Olympic kufanyika mwaka huu.

Japokuwa mashindano ya Olympic yatafanyika bila uwepo wa mashabiki kutoka nchi zingine, bado suala la kuruhusu mashabiki kutoka Tokyo pekee kuhudhuria mashindano hayo halijafikiwa maamuzi mpaka ifikapo mwezi Juni, 2021.

Akizungumza na BBC Sports, Naomi Osaka amesema ” Mimi ni mwanamichezo, kiuhalisia mawazo yangu ni kucheza Olympics. Lakini kama binadamu, ninaweza kusema tupo kwenye janga. 

Naomi Osaka, Naomi Osaka Hana Uhakika na Olympics., Meridianbet
Williams (kushoto) alitolewa na Osaka (kulia)kwenye nusu fainali ya Australian Open 2020.

“Kama afya za watu zipo hatarini na hakuna usalama, ninaweza kusema hiyo ni changamoto. Sina uhakika kama ni sahihi kufanyika mashindano ya Olympics wakati huu wa janga la COVID19.”

Wakati Naomi Osaka akiwa na mashaka na Olympics, Serena Williams bado hajaamua kama atashiriki mashindano haya ambapo yalipangwa kufanyika mwaka jana ila yaligharishwa kutokana na janga la COVID19.

Kwa Serena, vitu vingi vinahusika. Malezi ya mtoto wake, uwepo na janga la Corona, wingi wa mashindano anayofikiria kushiriki. Vyote hivi ni vitu ambavyo bado anafikiria kimoja baada ya kingine kabla ya kufanya maamuzi.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Naomi Osaka, Naomi Osaka Hana Uhakika na Olympics., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa