Kei Nishikori, nyota wa zamani namba nne duniani na mshindi wa medali ya shaba Olimpiki, ameaga mashindano ya Washington Open baada ya kupigwa seti mbili safi na kijana chipukizi Rafael Jodar. Katika mkutano wao wa kwanza kabisa kwenye ATP Tour, Jodar alishinda kwa urahisi 6-3, 6-2 na kufuzu robo fainali. Kwa mashabiki vijana, hii ni hadithi ya kizazi kipya kinachochukua nafasi huku kizazi cha zamani kikikaribia kufunga pazia.

Nishikori, mwenye miaka 36, tayari ametangaza kwamba atastaafu mwishoni mwa msimu wa 2026. Baada ya miaka ya kupambana na majeraha na changamoto za mwili, ameamua kuhitimisha safari yake ya kipekee. Kwa mashabiki wa tenisi, Nishikori atabaki kumbukumbu ya kiungo wa kiufundi aliyewahi kufika fainali ya US Open na robo fainali ya Wimbledon 2011.
Kwa upande mwingine, Jodar mwenye umri wa miaka 19 anaendelea kuandika jina lake kwenye ramani ya tenisi. Akiwa nafasi ya 24 duniani, kijana huyu aling’aa kwenye msimu wa clay mwaka huu kwa safari ndefu Barcelona, Madrid, Rome na Roland Garros. Ingawa alikwama Wimbledon, sasa ameanza swing ya hard-court Amerika Kaskazini kwa kishindo, akiwashinda Arthur Fils na Nishikori.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Robo fainali itamkutanisha Jodar na Lorenzo Musetti, mpinzani ambaye hajawahi kumkabili. Musetti, aliyepungua nafasi hadi namba 15 duniani baada ya majeraha ya paja, anarudi kwa mara ya kwanza tangu Italian Open. Washington imekuwa jukwaa lake la kurudi, akipita Matteo Arnaldi kwa walkover na kumshinda Aleksandar Vukic kwa seti tatu.

Kwa Jodar, ushindi huu ni hatua nyingine kuelekea taji lake la pili mwaka huu baada ya kutwaa Marrakech. Kwa Nishikori, ni ishara ya safari ya mwisho ya heshima. Kwa mashabiki wa tenisi Duniani kote, hii ni hadithi ya kizazi kinachopokezana mikoba, Jodar akipanda juu, Nishikori akishuka kwa heshima.


