Kunako muendelezo wa Roland Garros, almanusura Novak Djokovic ayaage mashindano mbele ya kijana wa miaka 19 raia wa Italia.
Djokovic alijitutumua kupindua matokeo yaliyomnusuru asiyaage mashindano ya French Open katika mzunguko wa 4 akichuana na Lorenzo Musetti. Mchezaji namba 1 kwa ubora duniani, alijikuta akizidiwa uwezo kabla ya kujipinda kurudi mchezoni na kumaliza mchezo kwa matokeo ya seti 6-7 (7-9) 6-7 (2-7) 6-1 6-0 4-0 baada ya Musetti kuumia.

Hii ni mara ya 5 Novak Djokovic anapindua matokeo akiwa tayari ameshapoteza seti 2 za awali. Hakika Novak ni mzoefu wa suala hili, japokuwa Musetti alionesha uwezo wake wa kupambana na Novak, maumivu ya misuli ya tumbo na mgongo, yalimfanya mchezaji huyo kulazimika kuacha kucheza na ushindi kwenda kwa Novak ambaye sasa anatinga hatua ya robo fainali.

Kwingineko kunako French Open 2021, Rafael Nadal amefuzu hatua ya robo fainali baada ya kumuadhibu Jannik Sinner kwa matokeo ya seti 7-5 6-3 6-0. Novak Djokovic atachuana na Matteo Berrettini huku Nadal akipambana na Diego Schwartzman katika michezo ya robo fainali.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.
magdalena
Bahati ilikuwa kwake