Emma Raducanu, bingwa wa zamani wa US Open na mchezaji nambari moja wa Uingereza, ataanza kampeni yake ya Wimbledon kwa mtanange wa kuvutia dhidi ya Mimi Xu, ambaye amepewa tiketi ya mwaliko. Mechi hiyo ya raundi ya kwanza inatarajiwa kuwa ya kusisimua hasa kwa kuwa inawakutanisha mabingwa wawili chipukizi wa nyumbani.

Katika upande wa wanaume, mchezaji bora wa Uingereza Jack Draper anayeshikilia nafasi ya nne duniani, naye anakabiliwa na ratiba ngumu. Ikiwa atafuzu hatua za awali, anaweza kukutana na bingwa mara saba wa Wimbledon, Novak Djokovic, katika robo fainali. Djokovic anawania rekodi ya kipekee ya ushindi wa 25 wa taji kubwa la Grand Slam.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa ujumla, idadi ya Waingereza waliomo kwenye droo ya michuano ya mchezaji mmoja mmoja mwaka huu imefikia 23, kiwango ambacho hakijashuhudiwa tangu mwaka 1984 huku Raducanu na Draper wakiwa wanaongoza kikosi hiki.

Ratiba ngumu kwa wachezaji wanawake wa Uingereza
Iwapo Raducanu atamshinda Xu katika raundi ya kwanza, atakutana na mshindi kati ya bingwa mtetezi wa mwaka 2023 Marketa Vondrousova na mchezaji aliyepewa nafasi ya 32, McCartney Kessler. Katika raundi ya tatu, anaweza kukutana na mchezaji nambari moja duniani, Aryna Sabalenka.
Wachezaji wengine chipukizi wa Uingereza waliopata tiketi za mwaliko ni Hannah Klugman na Mika Stojsavljevic, ambao pia wameangukia mikononi mwa wapinzani walio kwenye nafasi za juu. Klugman mwenye umri wa miaka 16 atakutana na Leylah Fernandez kutoka Canada, bingwa nambari 29, ambaye Raducanu alimshinda katika fainali ya US Open mwaka 2021.
Mika Stojsavljevic, bingwa wa US Open kwa vijana na pia mwenye umri wa miaka 16, ataanza dhidi ya Ashlyn Krueger wa Marekani, aliyepangwa nafasi ya 31.
Katika jumla ya wachezaji 10 wa Uingereza waliopo kwenye droo ya wanawake, nusu yao wamepangwa kukutana na wapinzani walio kwenye nafasi za juu, ishara ya changamoto kubwa kwa upande wa wenyeji.

Katie Boulter, ambaye alishikilia nafasi ya juu kabla ya Raducanu kumpiku mapema mwezi huu, atakutana na Paula Badosa wa Uhispania, mchezaji wa tisa kwa ubora. Sonay Kartal, mchezaji wa tatu kwa ubora Uingereza atamenyana na Jelena Ostapenko kutoka Latvia aliyepangwa nafasi ya 20. Heather Watson, mwenye umri wa miaka 33 atakabiliana na Clara Tauson wa Denmark aliyepangwa nafasi ya 23.
Mashindano ya Wimbledon mwaka huu yanatazamiwa kuwa na ushindani mkali, hasa kwa wachezaji wa nyumbani, ambao watalazimika kuonyesha uwezo wao mapema dhidi ya upinzani mzito.

