Rodger Federer Kuikosa Australian Open 2021.

Habari mbaya kwa mashabiki wa mchezo wa tenesi. Rodger Federer atayakosa mashindano ya Australian Open kwa mara ya kwanza baada ya miaka 22.

Rodger Federer bado anaendelea na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili akiwa nje ya uwanja toka mwezi Januari 2020.

Federer alitarajia kurejea uwanjani kwenye mashindano ya Australian Open ambayo yamesogezwa mbele mpaka Februari 8, lakini kutokana na afya yake atashindwa kuhudhuria mashindano hayo.

Federer ameshiriki mashindano ya Australian Open kwa miaka 21 mfululizo lakini kutokana na hali yake, wakala wa bingwa huyu wa Grand Slam mara 20 amesema “ni uamuzi sahihi utakaoleta matokeo chanya ya muda mrefu.”

Djokovic (kushoto) akipambana na Federer (kulia) kwenye nusu fainali ya Australian Open 2020.

Taarifa rasmi kutoka kwa mkurugenzi wa Melbourne – Craig Tiley amesema, ” Rodger yupo nyuma ya muda kwa ushiriki wake kwenye mashindano ya Grand Slam”.

Mchezo wa mwisho kwa Federer ilikuwa ni nusu fainali ya Australian Open ambapo alipoteza kwa bingwa wa mwaka huu (2020) – Novak Djokovic.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

10 Komentara

    Pole sana federer

    Jibu

    Pole Sana federer mwenyezi mungu amfanyiye wepesi apone majeraha alinayo ili arudi kwenye hali yake ya zamani

    Jibu

    Federer pole sana

    Jibu

    Bila Nadal mashndano yatapoa sana

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Sad news

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Duu pole yake

    Jibu

    Federer ni noma sana

    Jibu

    pole yake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.