Roger Federer Atangaza Kustaafu

Mchezaji nguli wa Tennis Roger Federer ametangaza kuachana na mchezo huo na kwamba mashindano ya ATP TOUR ya Laver Cup yatakuwa ya mwisho kwake na pia hatocheza mashindano yoyote makubwa (Grand Slams)

Federer (41) raia wa Switzerland anabaki kuwa mchezaji bora kwa wanaume kuwahi kutokea kwenye mchezo huo.

Roger Federer Alikuwa mcheza Tennis mwanaume wa Kwanza kutwaa mataji 20 ya Grand Slams, rekodi ambayo ilidumu sana na baadae kufikiwa na Rafael Nadal mwenye Grand Slams 22 na Novak Djokovic mwenye Grand Slams 21.

Mwaka mbaya kwa wapenzi wa tennis baada ya Gwiji mwingine kwa upande wa wanawake Serena Williams (40) kutoka USA nae kuachana na mchezo huo.

Roger anasema atacheza sana Tennis Lakini sio ile ya kiushindani tena. Kwa miaka 3 sasa amekuwa kwenye changamoto za majeruhi na kufanyiwa upasuaji mara kwa mara hali iliyomuondoa kwenye tennis ya ushindani kwa muda sasa.

Acha ujumbe