Bado matokeo yanaendelea kwenye kinyume na uwezo wa Serena Williams kuelekea mashindano ya French Open.
Baada ya kutolewa mapema kwenye mashindano ya Italian Open, Williams alikubali kupewa kadi maalumu ya kushiriki mashindano ya Emilia Romagna Open. Hata hivo, matokeo ya mchezo wa awali yameweka doa kwenye safari ya Serena Wililiams kuekelea French Open, 2021.
Williams amejikuta akiambulia kipigo cha seti 7-6 (7-4) 6-2 kutoka kwa Katerina Siniakov. Williams anawiki 2 tu za kujiandaa kuelekea mashindano ya French Open (Roland Garros) ambayo yataanza rasmi Mei 30, 2021.

Williams hana ratiba ya kucheza mchezo wowote kuelekea mashindano ya French Open ambapo atakuwa akiwania taji lake la 24 kwenye Grand Slam. Mpaka sasa, Williams ameshapoteza fainali 3 za Grand Slams wakati akitafuta namna ya kuifikia rekodi inayoshikiliwa na Margaret Court (mataji 24).
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.