Mchezaji nguli wa mchezo wa tenisi – Martina Navratilova, amesema kukosekana kwa baadhi ya wachezaji nyota kwenye Mashindano ya US Open mwaka huu, hakuyashushi kiwango mashindano hayo.
Kuelekea mashindano hayo ambayo yataanza Agosti 31, wachezaji nyota kutoka mataifa mbalimbali hawatoshiriki kutokana na sababu mbalimbali.
Kwa upande wa wachezaji wanawake, nyota 6 kati ya 10 bora duniani hawatoshiriki Mashindano ya US Open mwaka huu. Kwa upande wa wachezaji wanaume, wachezaji 3 watakosekana.
US Open 2020 kuwakosa wachezaji nyota wa tenisi.
“Sitoona utofauti wa washindi, tulishajua muda mrefu kwamba 2020 ni tofauti, kila mtu anapitia hali hii, tutaona ni nani ataitumia vizuri.” amesema bingwa mara 18 wa Grand Slam – Martina Navratilova.
Kwa upande wa wanawake, Andreescu, Ashleigh Barty, na bingwa mtetezi wa Wimbledon – Simona Halep ni kati ya watakaokosekana kwenye Mashindano ya mwaka huu.
Bingwa mara 6 – Serena Williams atakuwa uwanjani kulisaka taji la 24 la Grand Slam katika mashindano ya mwaka huu. Bingwa wa mwaka 2018 – Naomi Osaka nae atashiriki michuano ya mwaka huu.
Kwa upande wa wanaume, Rafael Nadal, Gael Monfils pamoja na Rodger Federer (majeruhi) hawatoshiriki mashindano ya mwaka huu. Bingwa namba 1 – Novak Djokovic, atakuwa uwanjani kulitafuta taji la 18 la Grand Slam.
Martina ameongeza kuwa, “Itakuwa ni rahisi kiasi kwa washindi kutokana na kutokuwepo kwa baadhi ya wachezaji nyota mwaka huu hasa upande wa wanawake. Unaweza kuwa na wachezaji nyota wote na bado ikatokea mshindi hajakutana na hata mmoja wa wachezaji hao.”
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


Shan
Habar njema!
Adelta
Good news 👍@meridianbettz
Sabrina
Hawatashuka kiwango lakini hakuta kuwa na motisha Kama ilivyokua hapo awali
Ester jackson
Kwa wachezaji watakao shiriki kweli haziwezi kushuka kiwango hata kama mashabiki hawatakuwepo bado Hadhi yake itabaki kuwepo
Khadija
tuangalie kama kweli watashuka kiwango kwa huu msimu wa 2020
Dorophina
Hawatoshuka kiwango lakini Kuna vitu vitapungua kwa kukosekana kwa hao watu maarufu na ndio watu huwa wanapenda kuwaangalia sana
Caroline
Inabidi wajitaidi maana hao wazoefu nao wana umuhimu wao
rama
vizuri sana
Zeiyana
Kuna baadhi ya vitu vitapungua ila kwa kiwango sizani kama kitaweza kushuka kwa wachezaji hao nguli wa tennis
Mwanahamisi
Gud news
Nasra
Gud news
Sauda
Inabidi wajitahidi sana
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri wapambane sasa
farida ahmadi
Kikubwa kujiweka sawa kujipanga vizuri
Mwajumah
Inabidi wajitaidi sana
Theonestina
Habari njema
David Pere
Hawatoshuka kiwango lakini Kuna vitu vitapungua kwa kukosekana kwa hao watu maarufu na ndio watu huwa wanapenda kuwaangalia sana
magdalena
habari nzuri sana zinasisimua
warda
Safi Sana
Tatu
Hili ni jambo nzuri
felister
motisha haitokuwepo
neema hassan
Gud newz
Samiah
Gud news