Taylor Townsend Aitikisa US Open Amtoa Mirra Andreeva

Taylor Townsend ameshika vichwa vya habari duniani baada ya kumtupilia mbali nyota chipukizi na mchezaji namba tano kwa ubora, Mirra Andreeva, katika raundi ya tatu ya US Open.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 29 alijikuta akizungumziwa kila kona baada ya Jelena Ostapenko kumkabili kortini mara tu baada ya mechi yao ya raundi ya pili na kumtuhumu kwa maneno makali akisema hana elimu wala heshima.

Taylor Townsend Aitikisa US Open Amtoa Mirra Andreeva

Kauli hizo zilizua mjadala mkubwa huku wachezaji wenzake wakimkingia kifua, baadhi wakihusisha matamshi hayo na ubaguzi wa rangi, madai ambayo Ostapenko alikanusha vikali.

Townsend alipewa nafasi ya kucheza kwenye jukwaa kuu la Arthur Ashe Stadium siku ya Ijumaa usiku na akajibu vyema kwa ushindi wa 7-5, 6-2 dhidi ya Andreeva.

“Kweli hii inahisi vizuri sana,” aliwaambia mashabiki baada ya mechi. “Kitu pekee nitakachosema ni, Karibuni kwenye onyesho. Najisikia vizuri ajabu. Najivunia kwamba nimeweza kuweka malengo yangu mbele ya yote.”

Aliongeza: “Nataka kuwashukuru wote walionipa sapoti katika masaa 48 yaliyopita. Hii ni zaidi yangu mimi peke yangu. Ni kuhusu ujumbe, ni kuhusu uwakilishi, ni kuhusu ujasiri wa kuonyesha wewe ni nani, na leo nimefanya hivyo. Mmemuona Taylor Townsend halisi.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Taylor Townsend Aitikisa US Open Amtoa Mirra Andreeva

Akizungumza na wanahabari baadaye, Townsend alisema hakuwa na presha kwenye mchezo huo. “Sikuwa na ugumu wowote. Niliwambia timu yangu, ‘Nimeumbwa kwa mambo kama haya’. Sikuwa na haja ya kujitetea kwa chochote kwa sababu nimesimama kwenye ukweli wangu. Sitaacha drama za nje zinipotoshe kutoka kwenye malengo yangu.”

Townsend pia alieleza namna alivyoshughulikia wimbi la ujumbe na maoni mitandaoni:

“Nilipoingia hotelini, nilijiambia, ‘Nimechoka sasa’. Nikaweka simu yangu chini na kuiweka kwenye do not disturb.”

Hii si mara ya kwanza Townsend anakabiliana na changamoto nje ya uwanja. Mwaka 2012, akiwa na umri wa miaka 16 na akiwa mchezaji bora wa vijana duniani, alizuiwa kushiriki US Open kwa sababu ya uzito wake. Amezungumza wazi kuhusu changamoto za mwili na safari yake ya kurejea kwenye hali bora ya kiafya baada ya kujifungua mtoto wake mwaka 2021.

Ushindi huu ni wa kihistoria kwake, kwa mara ya kwanza baada ya miaka sita amemshinda mchezaji wa Top 5 kwenye mashindano makubwa na kufuzu raundi ya nne ya Grand Slam.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.