Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi 3, Roger Federer aanza maandalizi ya Wimbledon kwa ushindi dhidi ya Ilya Ivashka.
Federer amerejea uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kujitoa kwenye mashindano ya French Open ili ajiimarishe vizuri kiafya.
2020 ulikuwa ni mwaka mbaya kwa Federer baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mara 3. Kuelekea mashindano ya Wimbledon, bingwa mara 20 wa Grand Slam ameibuka na ushindi wa seti 7-6 (7-4) 7-5 kunako Halle Open inayoendelea nchini Ujerumani. Federer anashikilia rekodi ya kubeba taji la mashindano hayo mara 10.
Federer atakutana na Felix Auger-Aliassime au Hubert Hurkacz kwenye mchezo unaofuata. Endapo atafuzu, naweza akakutana na Daniil Medvedev kwenye robo fainali.
SHINDA TSH 150,000,000/=
Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑
magdalena
Kazi nzuri