Wimbledon Yasogezwa Mbele Hadi 2021

Kwa mara ya kwanza tangu vita ya pili ya dunia, mashindano ya tennis ya Wimbledon hayatakuwepo mwaka huu kutokana na janga la Virusi vya Corona(covid19).

Mashindano ya Wimbledon yalitakiwa kuchezwa kati ya Juni 29 hadi Julai 12 mwaka huu. Wimbledon yanakuwa mashandano makubwa ya michezo kwa hivi karibuni kufutwa mwaka huu, baada ya Euro 2020 na Olimpiki ya Tokyo 2020. Ikumbukwe pia Mashindano makubwa ya French Open yaliyokuwa yamepangwa kuanza mwezi Mei, yameahirishwa hadi Septemba 20 mwaka huu.

“Maamuzi haya yameamuliwa kwa uangalifu mkubwa sana, na tumefikiria zaidi juu ya afya ya wafuatiliaji wetu na wale wote tunao kusanyika nao na kupelekea Wimbledon kutokea” Hayo yamesemwa na Ian Hewitt, Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Tennis nchini Uingeleza

Ian Hewitt

Chama cha Tennis nchini humo hakikutaka kufanya maamuzi hayo kabla ya kuisha kwa mwezi wa nne lakini muhtasari wake ulisha andaliwa kabla. Hiyo ni baada ya kukamilisha maandalizi yote na kua tayari kuwapokea watazamaji/wafuatiliaji wa michezo hiyo zaidi ya 40,000 katika viwanja mbali mbali.

Lakini selikari ya uingeleza imeshauri kuzuia mikusanyiko ya watu wengi kitu ambacho kingehatarisha afya za watu kwa wakati mmoja. Hata hivyo inatazamiwa hali ya huduma za afya nchini humo inaweza kua kawaida kati kati ya msimu wa joto.

Michezo yote ya Uingeleza imesimamishwa na vilabu vya michezo yote haviruhusiwi kuendelea na harakati zozote za kimichezo mpaka hali itakapo kua shwari.

Kukatishwa kwa ratiba katika michezo ya Wimbledon sio njia iliyozoeleka kabisa hivyo viongozi wameona bora kuanza upya kabisa michezo hiyo itakapo fika 2021.

 

2 Komentara

    Duh ipo POA sana

    Jibu

    Sio mbaya tutaisubiria tyuu mashabiki

    Jibu

Acha ujumbe