Wachezaji kutoka mataifa ya Urusi na Belarus hawataruhusiwa kushiriki na kucheza kwenye mashindano ya  Wimbledon mwaka huu kutokana na uvamizi waliofanya kwenye nchi ya Ukraine.

Miongoni mwa wachezaji maarufu ambao wataathiriwa na zuio hili ni mshindi wa U.S. Open Daniil Medvedev, ambaye kwa sasa anashika namba 2 duniani, pia mchezaji namba 8 kwa ubora duniani Andrey Rublev watakosa mashindano hayo.

Wimbledon, Wimbledon Kuwazuia Wachezaji kutoka Urusi na Belarus, Meridianbet

Kwa upande wa wanawake ambao watakosa mashindano ya Wimbledon ni Aryna Sabalenka ambaye anashika namba nne na alifikia nusu fainali ya mashindano hayo mwaka jana, Victoria Azarenka mshindi mara mbili wa  Australian Open na Anastasia Pavlyuchenkova mshindi wa pili wa mashindano ya French Open mwaka jana.

Medvedev, Rublev na Pavlyuchenkova hawa wote wanatoka Urusi wakati  Sabalenka na Azarenka wanatoka nchini Belarus.

Mashindano ya Wimbledon yanatarajiwa kuanza June 27. The All England Club walithibitisha mwezi march kuwa walifanya mazungumzo na serikali ya Uingereza kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa kwa wachezaji wa tenesi kutoka mataifa ya Urusi na Belarus kwenye mashindano ya Grand Slam.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa